
Hii ni moja kati ya
zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu na kesi hii ilianza toka
mwaka 2007 ambapo serikali ilitishia kulifungia gazeti la kanisa katoliki
endapo lingeendelea kumuita Mungu Allah.
Taarifa mpya ya sasa
inasema Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa katoliki
nchini humo kumuita Mungu ‘Allah’ kwenye gazeti linaloandika habari zake kwa
lugha ya Ki malay.
Walidai kuwa Wakristo
wanawakanganya Waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa
ambapo uamuzi wa Mahakama ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria
za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na kusababisha mashambulizi
katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh mwaka
2010.
Shirika la habari la ulimwengu
BBC wanaripoti kwamba Wakristo na wasikh
wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu ‘Allah’ katika lugha za kiMalay na
Sansrit kwa muda mrefu sana.
Mahakama nayo
imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo
ambapo mgongano huu kuhusu neno hilo moja umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye
dini na kabila tofautitofauti lilivyogawanyika.
Wanaharakati wa kiislamu
wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya Mahakama huku wengi wao wakiwa wanaamini
kuwa wakristo wanamwita Mungu ‘Allah’ kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge
na ukristo, shutma ambazo wakristo wamekana.
No comments:
Post a Comment