Tuesday, April 24, 2012

Waandamana Nusu Uchi Kulalamikia Polisi



Wanawake Uganda
Kundi la wanawake  nchini Uganda wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.

Tukio hilo lilisababisha kuwe na  ghadhabu ya umma ambapo pia lawama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawake katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.

Wanawake Michezoni

Mary Keitany

Wilson Kipsang

Kipsang na Keitany

Kipsang alikaribia kuvunja rekodi ya mashindano ya London Marathon
Wilson Kipsang na Mary Keitany kutoka Kenya walichukua ushindi kwa kishindo katika mashindano ya Jumapili ya mbio za London Marathon mwaka 2012.
Katika mbio za wanaume, Kipsang aliweza kuongoza katika maili saba za mwisho, na ilikuwa nusra avunje rekodi ya mashindano ya London.
Alimaliza kwa muda usiokuwa rasmi wa saa 2:04.44.
Mkenya mwenzake Martin Lel alifanikiwa kumpita mwanariadha wa Ethiopia, Tsegaye Kebede, na ambaye ameshawahi kuwa mshindi wa mashindano ya London, na kumaliza katika nafasi ya pili, katika kasi ya juu mno katika kumalizia mashindano.
Keitani amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa London Marathon
Kebede, aliyemaliza wa tatu, alifanikiwa kuwazuia Wakenya kuzoa nafasi zote tatu za mwanzo kwa upande wa mbio za wanaume, lakini kwa upande wa kina dada juhudi za Waethiopia hazikufanikiwa.
Mary Keitany alifanikiwa kuhifadhi ubingwa wake kwa mwaka wa pili mfululizo, kwa kushinda katika muda wa 2:18.37.
Muingereza wa kike aliyefanya vizuri zaidi ni Claire Hallissey, na alifanikiwa kufuzu kuingia mashindano ya Olimpiki.
Paula Radcliffe na Mara Yamauchi tayari walikuwa wamefuzu. kwa hisani kubwa ya BBC

Wivu wa Mapenzi Amuunguza Kwa Pasi ya Moto Mkewe

Wivu wa Mapenzi Amuunguza Kwa Pasi ya Moto Mkewe

NewsImages/6373006.jpg
Mke wa Henry baada ya kuunguzwa vibaya na moto wa pasi
Mwanaume mmoja wa nchini Nigeria anashikiliwa na polisi kwa kumuunguza na pasi ya moto mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwemo sehemu zake za siri kwa kile kilichodaiwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake mzazi.

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Henry Nnamdi mkazi wa jiji la Lagos nchini Nigeria, alimuua mtoto wake mchanga kwa kukibamiza kichwa chake kwenye sakafu mpaka alipofariki.

Henry hakuishia hapo alimchukua mke wake wa ndoa yao ya miaka miwili na kumfunga na kamba kwenye kiti kabla ya kutumia pasi ya moto kumuunguza mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake.

Henry alimuunguza vibaya mkewe kwenye matiti yake na sehemu zake za siri na sehemu mbali mbali za mwili wake kiasi cha kumfanya mkewe apoteze fahamu na hajazinduka hadi sasa.

Chanzo cha yote ni wivu wa Henry kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake Henry na kwamba huyo mtoto wake mchanga si mtoto wa damu yake kibailojia.
Henry anamtuhumu baba yake mzazi kutembea na mkewe.

Tukio hilo lililoutikisa mji wa Lagos, lilitokea wakati wa sherehe za pasaka mwezi huu ambapo majirani wa kitongoji cha Okota walishtushwa usiku usingizini na kelele za kuomba msaaada za mke wa Henry aliyejulikana kwa jina moja la Nnamdi.

Mke wa Henry huku akilia kwa uchungu wa maumivu ya kuunguzwa na moto wa pasi, aliwaita majirani waje kumuokoa.

Baada ya majirani kusita sita kuingia ndani ya nyumba ya Henry, walilazimika kuvunja mlango na kuingia ndani baada ya kelele za maumivu za mke wa Henry kuzidi.

Waliyoyashuhudia ndani baadhi walishindwa kuyangaalia kwa mara ya pili waligeuza njia na kurudi walikotoka na kwenda kuwaita polisi.

Polisi waliwahi kufika na kumkuta mke wa Henry akiwa amezimia hajitambui na maiti ya mtoto wake mchanga ikiwa kwenye sakafu.

Henry alikamatwa na kutiwa mbaroni huku mkewe akiwahishwa
hospitali ambako madaktari hadi sasa wanapigania maisha yake ingawa bado fahamu zake hazijamrudia.

Baba yake Henry amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mwanae akisisitiza kuwa mwanae atakuwa amehisi hivyo kwakuwa siku zote alikuwa akimpinga tabia yake ya kumnyanyasa na kumpiga mkewe. Majirani wengi wanamuunga mkono baba yake Henry kuwa ni mtu mzuri na hawezi kumsaliti mwanae na kulala na mkewe.

Henry anaendelea kushikiliwa na polisi.



TANGO: Kinga ya saratani zote, ni dawa ya ngozi

habareeeee, mi napenda saana kula matunda yasiyo na ladha ili kuepusha sukari isyo na tija mwilini. na tango ni moja ya matunda niyapendayo na tena nilile bila kumenya ila liwe limeoshwa vizuuuri.

Leo tunaangalia faida za tango kiafya. kama kuna mtu hajawahi kulila, kama yupo namshauri aanze leo.nikiwa na sababu za msingi kabisa nazo ni hizi!Tango lina virutubisho vingi na madini muhimu sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, miongoni mwa virutubisho na madini mengine yaliyomo, tango ni chanzo kizuri cha Kashiamu (IRON), ama  Chuma, Phosforas, Potasiamu, Zinki, Kambalishe, Vitamini B complex, Vitamini C na Vitamin E.

Unaweza kusema kuwa kirutubisho cha ‘Potasiamu’ ndiyo chakula cha moyo, kwa sababu ‘potasiamu’ ndiyo inayouwezesha moyo kupiga mapigo yake ya kawaida na kuustawisha. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ‘potasiamu’ kama tango, ni muhumi sana kwa mtu mwenye matatizo ya moyo, presha ya kupanda na matatizo ya mapigo ya moyo.

Aidha, tango linaaminika kupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini ,tango huimarisha misuli ya mwili na bila kusahau husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Virutubisho vilivyomo kwenye tango pia, hutoa afueni kwa mtu mwenye matatizo ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo. Wataalamu wetu wanatueleza pia kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.

Vile vile, tango lina kiwango kingi cha Vitamin C, hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa Vitamin C, kama vile kutokwa na damu kwenye fizi, upungufu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.

 faida kubwa kuliko zote  za kula tunda tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linatokana na ukweli kwamba tango lina kiwango kikubwa cha  (uchachu). Kwa kawaida ‘seli’ za saratani ‘haziwezi kuishi’ kwemye mazingira yenye uchachu, hivyo tango kinga ni kinga  dhidi ya saratani.

turejee zama za mababu kidogo, Tangu enzi na enzi, tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi, watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura zao. Hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara, hutengenezwa kutokana na tango.

Ulaji wa tango na unywaji wa juisi yake mara kwa mara, huondoa matatizo mengi ya ngozi yaliyomo ndani na nje ya mwili. Utakapotumia juisi ya tango kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo, utakuwa na ngozi nyororo na yenye afya kushinda hata mtu anayetumia vipodozi.

kama unataka kujaribu kunywa juice ya tango kama nlivyokwambia , Ni rahisi sana, chukua tango lako moja au zaidi, lioshe vizuri na limenye, kisha katakata vipande tayari kwa kusaga, ama kwa mashine  au kwa kutwanga kwenye kinu maalum, changanya na maji safi kiasi ili kupata juisi kiasi cha glasi moja.

Unaweza kuweka sukari kiasi kidogo sana kisizidi kijiko kimoja kwa glasi  ili kupata ladha au weka asali kijiko kidogo kimoja. Utapata matokeo mazuri na ya haraka kama ukinywa juisi yako kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.

Ili kutibu matatizo ya ngozi uliyonayo au magonjwa mengine kama tulivyoyaeleza hapo juu, kunywa juisi hiyo kwa muda wa wiki mbili hadi 4 mfululizo na angalia matokeo yake. Kwa  afya yako, weka mazoea ya kunywa japo mara mbili au tatu kwa wiki juice ya tango.

Vile vile, unaweza kujiwekea mazoea ya kula tango kwa njia mbalimbali kama vile kuchanganya na saladi, kachumbari au kutafuna lenyewe mara kwa mara, kwani faida zake mwilini ni nyingi anza leo.