Kipsang na Keitany
Kipsang alikaribia kuvunja rekodi ya mashindano ya London
Marathon
Wilson Kipsang na Mary Keitany kutoka Kenya walichukua ushindi
kwa kishindo katika mashindano ya Jumapili ya mbio za London Marathon mwaka
2012.
Katika mbio za wanaume, Kipsang aliweza kuongoza katika maili saba za
mwisho, na ilikuwa nusra avunje rekodi ya mashindano ya London.
Alimaliza kwa muda usiokuwa rasmi wa saa 2:04.44.
Mkenya mwenzake Martin Lel alifanikiwa kumpita mwanariadha wa Ethiopia,
Tsegaye Kebede, na ambaye ameshawahi kuwa mshindi wa mashindano ya London, na
kumaliza katika nafasi ya pili, katika kasi ya juu mno katika kumalizia
mashindano.
Keitani amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa London Marathon
Kebede, aliyemaliza wa tatu, alifanikiwa kuwazuia Wakenya kuzoa nafasi zote
tatu za mwanzo kwa upande wa mbio za wanaume, lakini kwa upande wa kina dada
juhudi za Waethiopia hazikufanikiwa.
Mary Keitany alifanikiwa kuhifadhi ubingwa wake kwa mwaka wa pili mfululizo,
kwa kushinda katika muda wa 2:18.37.
Muingereza wa kike aliyefanya vizuri zaidi ni Claire Hallissey, na
alifanikiwa kufuzu kuingia mashindano ya Olimpiki.
Paula Radcliffe na Mara Yamauchi tayari walikuwa wamefuzu. kwa hisani kubwa
ya BBC
No comments:
Post a Comment