Monday, June 23, 2014

BRAVOO



MUNGU NI WA WOTE NA ANA MAJINA LUKUKI




Hii ni moja kati ya zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu na kesi hii ilianza toka mwaka 2007 ambapo serikali ilitishia kulifungia gazeti la kanisa katoliki endapo lingeendelea kumuita Mungu Allah.

FIFA 2014 WORLD CUP



Monday, February 18, 2013

ALIYEMCHOMA MTOTO MKONO NA KUMLISHA KINYESI, ASWEKWA JELA MAISHA




Wilvina Mukandala (24) anayetuhumiwa kumnyanyasa mtoto wa dada yake aitwae Aneth Johannes (3) kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto mtoto huyo kisha kukatwa mkono hospitali, amehukumiwa kifungo cha maisha jela.Pichani kushoto ndiye mtuhumiwa mwenyewe akisomewa hukumu, kulia juu ni mtoto Aneth baada ya kuunguzwa, chini kushoto ni Aneth baada ya kukatwa mkono.

Wednesday, November 28, 2012

M23 sasa waondoka Goma


M23 wakiondoka Goma.
Kufuatia juhudi za kimataifa na mataifa jirani, hatimaye waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekubali kuondoka Goma na sasa wanakwenda kujikusanya kwenye mji wa Sake, nje kidogo ya Goma.

Tuesday, October 2, 2012

MAHABA NI SANAA INAYOJITEGEMEA!



 


je ulikutana wapi na mpenzi wako kwa mara  ya kwanza? hili ni jambo kubwa na la msingi! katika maisha yako ya kimapenzi na hata kwa kujiwekea kumbukumbu!
inawezekana mmekutana katika mazingira ambayo yanweza kukufanya ujisikie aibu ama udhalili fulani hivi, labda bar, msibani, kituo cha basi, kazini kwako, kwenye movie mloigiza pamoja,harusini ama kwingineko.
kwangu mimi haijalishi , ninachokusihi ni kusahau kumbukumbu mbaya akilini mwako na kuichukua hiyo kama historia na kuifanyia kazi na kulidumisha penzi lako kadiri unavyojaaliwa na changanya na kiasi cha ubunifu kidogo mambo yatakua mswano au mazuri.

Tuesday, April 24, 2012

Waandamana Nusu Uchi Kulalamikia Polisi



Wanawake Uganda
Kundi la wanawake  nchini Uganda wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.

Tukio hilo lilisababisha kuwe na  ghadhabu ya umma ambapo pia lawama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawake katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.