Tuesday, October 2, 2012

MAHABA NI SANAA INAYOJITEGEMEA!



 


je ulikutana wapi na mpenzi wako kwa mara  ya kwanza? hili ni jambo kubwa na la msingi! katika maisha yako ya kimapenzi na hata kwa kujiwekea kumbukumbu!
inawezekana mmekutana katika mazingira ambayo yanweza kukufanya ujisikie aibu ama udhalili fulani hivi, labda bar, msibani, kituo cha basi, kazini kwako, kwenye movie mloigiza pamoja,harusini ama kwingineko.
kwangu mimi haijalishi , ninachokusihi ni kusahau kumbukumbu mbaya akilini mwako na kuichukua hiyo kama historia na kuifanyia kazi na kulidumisha penzi lako kadiri unavyojaaliwa na changanya na kiasi cha ubunifu kidogo mambo yatakua mswano au mazuri.

 
namna ya kudumisha ni namna ya wewe utakavyo lithamini penzi lako na hii itakufanya wewe uonekane mpya kila siku kwa mpenzi wako, na valentain haitakua  mara moja kwa mwaka katika maisha yenu ya kimapenzi bali kila iitwapo leo!

                                Prince Williams na Kate Middleton's

mpende na kumuenzi mpenzio kwa kumpa ama kumbatiza majina mazuri mazuri ama kutokana na kilema chake cha asili pengine kama ana gubu na maneno maneno yasiyokwisha na amri za hapa na pale sana basi mwite kamanda! ama vyovyote uwezavyo!
 pia kabla mpenzio hajalala ama kupanda kitandani basi fanya kaubunifu kwa kutupiamo petals, unanunua ua waridi ama roses kama wenyewe waliitavyo na kulinyambua na kisha unatupiamo kitanda kizima na kisha unarudishia bed cover kisha weka maua ya asmini chumbani yatatoa harufu nzuri isiyokera na kisha unaendelea na hamsini zako.
mpenzio atakapoingia chumbani na kukutana na riha hiyo ataifurahia na atachanganyikiwa zaidi kwa petals atakazokutana nazo chini ya bedcover! utakua ume mu win na atakua wko maishani hakuna haja ya kumuendea kwa mganga wala nini!


                                               Mahaba ni kuya tengeneza

mahaba ni ubunifu kila uchao na wala usichoke! kila la kheri buni kivyako leo kisha nishirikisha mafanikio yako!

No comments:

Post a Comment